Klabu yetu leo imezindua rasmi kampeni ya kuchangisha fedha za kujenga uwanja wetu wa kisasa kwa ajili ya mechi zetu za nyumbani.
Wikiendi iliyopita Rais wa Heshima ambaye ni mwekezaji wa klabu, Mohamed Dewji (Mo) aliishauri Bodi ya Wakurugenzi kutangaza utaratibu wa kuchangisha wanachama na mashabiki huku yeye akiahidi kutoa Sh bilioni mbili kufanikisha ujenzi huo.
Advertisement
Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez wamezindua kampeni hiyo leo mbele ya wanahabari ambayo imepewa jina 'SIMBA YETU UWANJA WETU' kwa ajili ya kuhamasisha watu kuchangia.
Wanachama na mashabiki watachangia pesa kupitia mitandao ya simu ya Tigo, Vodacom, Airtel na benki ya NMB ambapo namba za kutumia tayari zimewekwa hadharani.