Simba Sports Club
News

Kakolanya: Nikipewa nafasi naitumia ipasavyo

15 Dec 2021

Mlinda mlango namba mbili, Beno Kakolanya ameweka wazi kuwa kila nafasi atakayopewa ya kucheza atahakikisha anafanya vizuri ili kuendelea kuaminiwa na benchi la ufundi.

Kakolanya amecheza mechi yake ya kwanza msimu huu jana dhidi ya JKT Tanzania katika michuno ya Azam Sports Federation Cup ambayo tuliibuka na ushindi wa bao moja.

Mlinda mlango huyo amemshukuru Kocha Pablo Franco kwa kumpa nafasi ya kucheza katika mchezo wa jana huku akiahidi kuonyesha uwezo wake kila atakapopangwa.

"Kwangu ulikuwa mchezo mzuri pia namshukuru mwalimu kwa kuniamini, namshukuru Mungu sikumuangusha pia nafikiri njia nzuri kwangu pale nitakapopata nafasi nionyeshe uwezo wangu ili niendelee kuaminiwa," amesema Kakolanya.

Advertisement

Kakolanya ameongeza kuwa Pablo ni kocha mzuri kuna vitu vipya anawafundisha na vingine vya zamani hivyo anaamini kama atapewa muda ataweza kuifikisha timu mbali.

"Kwangu Pablo ni mwalimu mzuri japo tumekaa naye siku chache, kuna vitu vipya anatufundisha vingine si vigeni kwa imani yangu nafikiri tutafika malengo ambayo yeye anayataka," amesema Kakolanya.

Kabla ya jana mara ya mwisho Kakolanya kudaka ilikuwa Juni 22 katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Back to homepage
Share this story