Kagoma amesema suala la kugombania namba lipo kwenye kila timu na hilo halimpi shida atapambana ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi.
Akizungumzia msimu ujao wa Ligi 2024/25 Kagoma amesema anaamini tutafanya vizuri kutokana na ubora na uimara wa kikosi tulionao.
"Ushindani kwenye kila timu hauepukiki kutokana na kuhusisha wachezaji wengi. Binafsi siogopi ushindani wa namba nipo hapa kwa ajili ya kupambana ili kuisaidia timu."
Advertisement
"Nafahamu mashabiki wa Simba wana matumaini makubwa msimu huu na tunajipanga kuhakikisha tunawapa furaha," amesema Kagoma.
Akizungumzia kuhusu uamuzi wa kuichagua Simba licha ya kutakiwa na timu nyingine Kagoma amesema "ndoto yangu ilikuwa kuichezea Simba tangu akiwa mtoto ndio maana alivyopata nafasi hakusita."