Daktari wa timu Edwin Kagabo amesema nyota hao wapo fiti kufanya mazoezi pamoja na wenzao.
Dkt. Kagabo ameongeza kuwa wawili hao wapo tayari kushuka dimbani katika mchezo wetu wa ligi unaofuata dhidi ya Coastal Union endapo mwalimu Fadlu Davids ataona inafaa.
Advertisement
"Mzamiru na Kagoma wamerejea mazoezini pamoja na wenzao na wapo tayari kwa ajili ya kucheza mechi. Majeraha yao yamepona na Sasa wapo tayari kuitumikia Simba," amesema Dkt. Kagabo.
Mzamiru alipata maumivu ya mguu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan mwezi Agosti huku Kagoma akipata maumivu kwenye mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahli Tripoli.