Simba Sports Club
News

Kagoma aongeza miwili

8 Mar 2026

Kagoma alijiunga nasi kutoka Singida Black Stars, Julai 2024 kwa mkataba wa miaka miwili ambayo ilikuwa inamalizika mwishoni mwa msimu.

Kutokana na uwezo mkubwa anaoendelea kuuonyesha Uongozi wa klabu baada ya kupokea taarifa kutoka benchi la ufundi umeridhia kumuongezea mkataba wa miaka miwili.

Advertisement

Uongozi unaendelea kuwaongezea mikataba mipya wachezaji ambao wapo kwenye mipango ya mwalimu kuelekea msimu ujao wa mashindano 2026/2027.

Back to homepage
Share this story