Washambuliaji wetu Medie Kagere na Bernard Morrison leo wamepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11.
Kocha Pablo Franco amekuwa akiamini matumizi ya washambuliaji wawili lakini mmoja akiwa asilia na mwingine kiungo mshambuliaji.
Kagere na Morrison watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Hassan Dilunga na Kibu Denis ambao watatokea pembeni.
Katika kiungo wa ulinzi Jonas Mkude na Sadio Kanoute wamepangwa eneo hilo huku Joash Onyango na Henock Inonga wakisimama kama walinzi wa kati.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Kibu Denis (38), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Bernard Morrison (3) na Hassan Dilunga (24).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19),
Peter Banda (11), John Bocco (22), Rally Bwalya (8), Yusuph Mhilu (27).