Mutale mwenye miaka 22 anamudu kucheza nafasi nyingi Uwanjani tena kwa ufanisi wa hali ya juu.
Joshua anaweza kumudu nafasi ya winga ya kulia, kushoto na wakati mwingine anacheza nyuma ya mshambuliaji yaani namba 10.
Akiwa Power Dynamos msimu uliopita, Mutale amefunga mabao nane na kuisaidia kupatikana kwa mengine 10 katika michezo 26.
Advertisement
Uwezo wake wa kumudu kucheza nafasi nyingi Uwanjani pamoja na umri ni miongoni mwa vigezo vilivyotuvutia kumsajili mchezaji huyo ikiwa ni mkakati maalumu wa kuboresha kikosi chetu kwa kusajili damu changa na wenye ubora
Joshua Mutale anakua ni mchezaji wa pili kusajiliwa ndani ya Simba baada ya Lameck Lawi na bado Wachezaji wengine wataendelea kusajiliwa na kutambulishwa