Simba Sports Club
News

Jinsi tulivyomaliza mzunguko wa kwanza Ligi ya NBC

2 Mar 2022

Wakati tunakwenda kuanza mzunguko wa pili tuko nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi tukiwa nyuma kwa alama 11 dhidi ya wanaongoza lakini tuna mchezo mmoja mkononi amnao tukishinda tutazipunguza na kubaki nane.

Hadi sasa tumefanikiwa kukusanya alama 31 baada ya kucheza mechi 15 tukishinda tisa, tukitoka sare nne na kupoteza miwili. Tumefunga mabao 16 na kufungwa sita.

KAGERE KINARA WA UFUNGAJI

Mshambuliaji Medie Kagere ndiye kinara wa ufungaji ndani ya kikosi chetu akifunga mabao matano akisaidia kupatikana kwa moja (assist) baada ya kucheza mechi 14 sawa na dakika 778.

Kagere anazidiwa mabao matano na kinara wa ufungaji hivyo kuelekea mzunguko wa pili matumaini ya kuwafikia walio juu ni makubwa.

Kibu Denis anafuatia kwa kufunga mabao matatu. Wengine ambao wamefunga bao moja kila mmoja ni:

Mohamed Hussein

Pape Sakho

Joash Onyango

Clatous Chama

Advertisement

Peter Banda

Sadio Kanoute

Mzamiru Yassin

MANULA NA CLEAN SHEET TISA

Mlinda mlango Aishi Manula, amemaliza mzunguko wa kwanza kwa kutoruhusu bao katika mechi tisa kati ya 15 alizocheza.

Manula amedaka dakika 1350 na kuruhusu nyavu zake kuguswa mara sita pekee.

MIPANGO YA MZUNGUKO WA PILI

Licha ya kuwa nyuma kwa idadi kubwa ya alama dhidi ya walio juu yetu bado lengo letu kuu ni kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu.

Mechi zetu zote 15 za mzunguko wa pili tukianza Ijumaa dhidi ya Biashara tutacheza kama fainali na tumejipanga kuhakikisha hatuangushi alama yoyote ili kutimiza malengo yetu kutetea ubingwa.

Back to homepage
Share this story