Simba Sports Club
News

Jentrix akabidhiwa kiatu cha ufungaji bora SLWPL

12 Jun 2023 By simbasc 184 views
Mshambuliaji Jentrix Shikangwa amekabidhiwa tuzo yake ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women's Premier League (SLWPL) 2022/23. Shikangwa amekabidhiwa kiatu cha dhahabu katika hafla ya tuzo za TFF 2022/23 zinazofanyika jijini Tanga usiku huu. Shikangwa pia amechaguliwa katika kikosi bora cha SLWPL msimu wa 2022/23. Wachezaji wengine walioingia kwenye kikosi bora cha msimu ni pamoja na walinzi Fatuma Issa 'Fetty Densa' na Violeth Nicholas.
Advertisement
Back to homepage
Share this story