Simba Sports Club
News

Jayrutty yatoa ofa ya jezi kipindi cha Sikukuu

16 Dec 2025

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema ofa hii imeanza rasmi leo Disemba 16 na kumalizika Januari 30/2026 zoezi ambalo litachukua siku 45.

“Tuko hapa kuwatangazia Wanasimba wote Tanzania na duniani kwamba tumetoa punguzo la bei ya jezi kutoka Tsh. 45,000 hadi Tsh. 12,000. Ofa hii ya sikukuu ni kwa jezi zote, za ligi, za kimataifa na za watoto. Jezi za watoto zimetoka na sasa zinapatikana madukani," amesema Ahmed.

Ahmed ameongeza kuwa “Namna ya kuipata jezi hii ya ofa itakuwa kwa njia ya mtandao, kwa watu wanaotumia smart off au kiswaswadu. Kuipata itakuwa kwenye website ya jayruttyshop.co.tz utanunua jezi yako na unaweza kuipata kwa kutumia mitandao ya simu.”

“Kupitia mitandao ya simu unaweza kununua ukitumia mtandao wowote ukilipa kwa namba ya 61223807 na baada ya hapo utakwenda kwenye ofisi ya Shirika la Posta au ofisi za JayRutty. Unaruhusiwa kununua jezi kwa idadi yoyote unayotaka. Kuchagua size au rangi utachagua hilo ukishafika ofisini kuchukua jezi zako," amesema Ahmed.

Advertisement

Ahmed ameongeza kuwa pamoja na kutoa ofa hiyo pia Uongozi wa klabu kwa kushirikiana na Jayrutty unaendelea kupambana na wauzaji wa jezi feki kote nchini.

"Pamoja na kwamba tunatoa punguzo la msimu wa sikukuu lakini pia tunapambana na jezi fake. Kama Mwanasimba alikuwa ananunua jezi feki Tsh. 15,000 sasa jezi original ataipata kwa Tsh. 12,000. Uamuzi ni kwako Mwanasimba."

"Unaweza kupata jezi hii hata kwa kukopa. Mitandao yote ya simu wanakopesha wateja wao hivyo unaweza kukopa sasa na kupata jezi yako. Hii fursa hatupaswi kuichezea hata kidogo, huu ndio wakati wa kila Mwanasimba kununua jezi yake original," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story