Simba Sports Club
News

Israel Patrick arejea mazoezini

16 Nov 2021

Mlinzi wa kulia Israel Patrick ameanza mazoezi leo baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua.

Israel alipata majeraha hayo akiwa katika kikosi chaTimu ya Taifa ya Tanzania kilichokuwa kinajiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo.

Advertisement

Kutokana na majeraha hayo Israel aliikosa safari ya Madagascar katika mchezo wa mwisho wa Stars kwenye michuano hiyo uliopigwa Jumapili iliyopita.

Licha ya kuanza mazoezi mlinzi huyo atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari ingawa ameingia kambini pamoja na wenzake kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting.

Back to homepage
Share this story