Nyota hao ni mlinzi wa kati, Henock Inonga kiungo mshambuliaji, Said Ntibazonkiza pamoja na mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe.
Mechi mbili za mwisho dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union zimechezwa Juni lakini zinahesabika ni za Mei kwakuwa zilizosogezwa mbele kutokana na ushiriki wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Takwimu za wachezaji wote katika mwezi Mei
Dakika Magoli Assisti
Inonga 180 0 0
Ntibazonkiza 450 7 5
Kapombe 360 0 3
Zoezi la kupiga kura limeanza leo kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litamalizika Jumatatu saa sita mchana.
Mshindi wa jumla atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.