Simba Sports Club
News

Inonga nje wiki mbili

15 Aug 2023

Inonga ameshindwa kuendelea na mchezo huo na kutolewa kufuatia kuumizwa bega na mshambuliaji, Medie Kagere.

Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema baada ya kufanyiwa vipimo mlinzi huyo hajapata madhara makubwa hivyo atakuwa nje kwa wiki mbili ili kuwa kamili kabisa.

Advertisement

"Inonga atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili ili jeraha lake la bega lipone kabisa, hakuumia sana lakini anapaswa kupumzika kwa muda kabla ya kurudi uwanjani ili kumkinga asipate madhara zaidi," amesema Dk. Kagabo.

Back to homepage
Share this story