Inonga hakuumia sana kama ilivyoonekana isipokuwa alichanika kidogo na ameshonwa hivyo atakuwa nje kwa muda huo.
Inonga alichezewa madhambi na mshambuliaji Samson Mbangula na kushindwa kuendelea na mchezo ambapo awali ilionekana ameumia vibaya na ingemchukua muda mrefu kupona lakini hali ni tofauti.
Advertisement
Mshambuliaji kinara Moses Phiri naye anaendelea vizuri na yupo mbioni kurejea uwanjani.
Winga Peter Banda ambaye kwa takribani miezi mitatu alikuwa nje ya uwanja akiuguza jeraha anaendelea vizuri akiwa ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa daktari.