Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema tumeamua kumpa heshima Inonga kwakuwa ndiye mchezaji pekee aliyeiwezesha timu yake ya DR Congo kumaliza nafasi ya nne kwenye michuano ya AFCON.
Ahmed amesema kwa sasa Inonga ndiye mchezaji mwenye hadhi kubwa kuliko wote ambao watakuwa uwanjani siku ya Jumamosi ndio maana tukaona anapaswa kuwa mgeni rasmi kwa ajili ya kuthamini anachokifanya.
"Jumamosi mgeni rasmi ni mlinzi wetu wa kati Henock Inonga kutokana na kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya nne kwenye michuano ya AFCON," amesema Ahmed.
Viingilio vya mchezo huo vitakuwa kama ifuatavyo:
Advertisement
Mzunguko ni Sh. 5000
VIP C Sh. 10,000
VIP B Sh. 20,000
VIP A Sh. 30,000