Simba Sports Club
News

Inonga, Chama waitwa timu zao za Taifa

15 Sep 2022

Inonga amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Congo DR inayonolewa na kocha Sebastian Desebre ambapo itacheza mechi mbili dhidi ya Burkina Faso na Sierra Leone.

Inonga ambaye ni beki bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita ndiye mchezaji pekee anayecheza ligi ya Tanzania kuitwa kwenye kikosi hicho.

Advertisement

Kwa upande wa Chama amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) ambacho kitacheza mechi mbili dhidi ya Libya na Mali.

Back to homepage
Share this story