Wawili hao wamepata alama nyingi kutokana na ubora waliouonyesha katika mchezo uliopita uliofanyika Juzi Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam dhidi ya Wydad Casablanca ambapo tuliiibuka na ushindi wa bao moja.
Hii si mara ya kwanza kwa wachezaji wetu kujumuishwa kwenye kikosi bora cha wiki kutokana na viwango wanavyoonyesha kwenye kila mchezo.