Simba Sports Club
News

Inonga atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora

4 May 2022

Ndani ya mwezi Aprili, Inonga amecheza mechi nne sawa na dakika 360 huku akionyesha kiwango safi kwenye michezo yote.

Inonga amewapiku walinzi wenzake Shomari Kapombe na Joash Onyango ambao aliingia nao fainali ya kinyang'anyiro hicho.

Baada ya kuibuka mshindi, Inonga atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa

Advertisement

Jina Kura Asilimia

Kapombe 457 16.49

Inonga 2277 82.14

Onyango 38 1.37

Back to homepage
Share this story