Inonga alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumizwa na Ugando dakika ya 20 kulikosababisha kuchanika juu kidogo ya kifundo cha mguu.
Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema Inonga ameshonwa nyuzi 13 katika jeraha hilo na tayari ameruhisiwa kurudi nyumbani.
Advertisement
"Inonga ameruhisiwa kutoka Hospitali, amepata jeraha pale pale ambapo aliumia katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons. Jambo zuri ni kwamba hajavunjika mfupa ni kidonda tu," amesema Dk. Kagabo.
Kuhusu kuwa atakuwa nje kwa muda gani Dk. Edwin amesema "itategemea na jinsi atakavyopona kidonda lakini haikuwa mbaya sana."