Simba Sports Club
News

Inonga akabidhiwa tuzo yake ya Emirate

3 Mar 2023

Inonga ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwapiku nyota wenzake Shomari Kapombe na Mzamiru Yassin ambao ameingia nao kwenye kinyang'anyiro hicho.

Katika mwezi Februari Inonga amecheza mechi tano (tatu za Ligi ya Mabingwa mbili za Ligi Kuu) sawa na dakika 450 akifunga bao moja dhidi ya Vipers.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Inonga amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompa benchi la ufundi pamoja na mashabiki kwa kumpigia kura kufanikisha kuibuka mshindi.

Akizungumzia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa Jumanne, Inonga amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuisapoti timu na wachezaji watahakikisha wanapambana kupata ushindi.

Advertisement

"Kwanza nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa, benchi la ufundi pamoja na mashabiki ambao wamenipigia kura zilizonipa ushindi huu, nawashukuru sana.

"Pia naomba niwasisitize mashabiki wetu mje kwa wingi uwanjani Jumanne, sisi wachezaji tupo tayari kuhakikisha tunawapa furaha," amesema Inonga.

Inonga amekabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 pamoja na tuzo kutoka kwa wadhamini wetu Emirate Aluminium Profile.

Back to homepage
Share this story