Simba Sports Club
News

Idara ya Habari yaendelea na kutangaza Utalii Zanzibar

6 Jan 2024

Tulianza kutembelea Makumbusho Ya Sanaa ambayo ndani yake kuna Baytil Amaan jengo lilojengwa baada ya vita Ya Kwanza Dunia ili kuwakumbuka na kuwaenzi wahanga wa vita hiyo iliyopiganwa kuanzia 1914- 1918.

Baada ya kutoka Makumbusho tulielekea Ngome Kongwe ambayo ilijengwa mwaka 1710 kwa ajili ya Ulinzi na Usalama wa waarabu baada ya kuwafukuza Wareno.

Tulikamilisha ziara kwa kwenda Mtoni Palace ambapo ni kasiri la kwanza la Mfalme wa Zanzibar, Sayed Said Bin Sultan sehemu Ya Kwanza Ya Kupandwa Karafuu.

Advertisement

Lengo la kutembelea katika sehemu hizo ni kujifunza mambo mbalimbali ya historia ya Zanzibar pamoja na kutangaza Utalii wa Visiwa hivi.

Jana Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Simai Mohamed Said aliitangaza klabu yetu kuwa balozi wa Utalii wa Zanzibar kutokana na maamuzi ya kuamua kutangaza Utalii wa Visiwa hivi kupitia Mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea.

Back to homepage
Share this story