Simba Sports Club

Honour Janza Mkurugenzi mpya wa Ufundi

27 Oct 2026

Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kumuajiri, Honour Janza (66) raia wa Zambia kuwa Mkurugenzi mpya wa Ufundi.

Ujio wa Janza umekuja kuongeza nguvu katika benchi la ufundi chini ya kocha Steve Barker kwa ajili kuongeza ufanisi ndani ya timu kwa ajili ya michuano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kabla ya kujiunga nasi Janza alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Zesco United ya Zambia ambapo alijiunga nayo tangu mwaka 2023.

Janza ana leseni B kutoka Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) na Leseni A ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Hizi hapa kazi alizofanya Janza kabla ya kujiunga nasi:

⏹️ 2009-2010 Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zambia chini ya umri wa miaka 20.

⏹️ 2011-2014 Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo'.

Advertisement

⏹️ 2014-2015 Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo'.

⏹️ 2009-2017 Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha soka cha Zambia.

⏹️ 2017-2018 Kocha mkuu wa timu ya Red Arrows

⏹️ 2019-2020 Kocha mkuu wa Mbabane Swallows

⏹️ 2020-2021 Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya NAPSA FC

⏹️ 2021-2022 Kocha mkuu wa timu ya Namungo FC

⏹️ 2023-2026 Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Zesco United.