Kajula amesema Simba sio ya Dar es Salaam pekee ndio maana tumeamua kuipeleka Wiki ya Simba Mikumi ili kuwapa nafasi mashabiki kutoka Morogoro kuwa karibu na timu yao.
Kajula ameongeza kuwa kwenda kuzindua Wiki ya Simba katika Mbuga ya Wanyama Mikumi itakuwa ni faida kwa Serikali pia kwakuwa tutatangaza Utalii wa nchi huku tukitumia treni ya mwendokasi (SGR).
"Simba sio ya Dar es Salaam pekee, Simba iko kila mahali ndio maana safari hii tunaenda Mikumi kuzindua Wiki ya Simba ili na mashabiki kutoka Morogoro," amesema Kajula.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja ameupongeza Uongozi wa klabu kwa kuamua kuunga mkono jitihada za Serikali ya kutangaza Utalii kwa kwenda kuzindua Wiki ya Simba katika Mbuga ya Wanyama Mikumi.
"Mmefanya jambo kubwa na kupongezwa, kuzindua Wiki ya Simba Mbugani ni kuunga mkono jitihada za Serikali kukuza Utalii.
"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliigiza filamu ya Royal Tour ili kukuza Utalii nanyi mnapita kule kule, kwa upande wetu TRC tutakuwa pamoja nanyi muda wote," amesema Kadogosa.
Nae Mhifadhi Mkuu wa Mikumi, Augustine Msesa amesema Uongozi wa klabu umewapa heshima kubwa Wanamikumi kushiriki tukio hilo kubwa na imani yake ni kwamba mashabiki wengi watajitokeza.