Viingilio vilivyowekwa ni rafiki kwa kila shabiki sababu tunafahamu ili Tamasha letu lifane tunahitaji watu wajitojeze kwa wingi.
Viingilio vimepangwa kama ifuatavyo:
Mzunguko Sh. 5000
Machungwa Sh. 10,000
VIP C Sh. 20,000
Advertisement
VIP B Sh. 30,000
VIP A Sh. 40,000
Platinum Sh. 200,000
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amewasisitiza mashabiki kununua tiketi mapema ili kuepusha usumbufu siku ya tukio.
Ahmed amesema matawi yanaweza kujipanga na kununua tiketi za jumla zitakazouzwa katika Ofisi za klabu kulingana na wingi wao ili kupunguza foleni.