Simba Sports Club
News

Hivi hapa Viingilio vya Simba Day

22 Jul 2024

Meneja Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema lengo la kuweka hadharani viingilio ni kuwapa nafasi mashabiki kununua mapema ili kuepuka usumbufu.

Ahmed amesema mwaka jana tiketi za Simba Day ziliisha siku mbili kabla ya tamasha lakini safari hii tumepanga ziishe siku tano kabla.

"Kikubwa mashabiki nunueni tiketi mapema ili kuepuka usumbufu, Simba hii sio ya kuitazama kwenye TV. Tiketi zitaisha mapema kwahiyo Wanasimba msichelewe kununua," amesema Ahmed.

Hivi hapa Viingilio vyenyewe:

Mzunguko Sh. 5000

Advertisement

Machungwa Sh. 10,000

VIP C Sh. 20,000

VIP B Sh. 30,000

VIP A Sh. 40,000

Platinum Sh. 200,000

Back to homepage
Share this story