Simba Sports Club
News

Hivi hapa viingilio vya mechi ya marudiano dhidi ya De Agosto

10 Oct 2022

Kiingilio cha chini kwenye mchezo huo kitakuwa Sh 3,000 ili kuwapa nafasi ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema tumeweka viingilio hivyo rafiki ili kuwafanya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu kufika hatua ya makundi kwa mara ya nne kwenye historia yetu.

"Tumetangaza viingilio hivi mapema na rafiki ili kuwafanya mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kuja kuishuhudia timu ikifuzu hatua ya makundi ambayo itakuwa ni mara ya nne," amesema Ahmed.

Viingilio hivyo vimepangwa kama ifuatavyo

Mzunguko Sh 3,000

Advertisement

Machungwa Sh 5,000

VIP C Sh 10,000

VIP B Sh 15,000

VIP A Sh 20,000

Back to homepage
Share this story