Simba Sports Club
News

Hivi hapa viingilio vya mchezo wa ufunguzi wa AFL

11 Oct 2023 By simbasc 185 views
Ufunguzi wa michuano ya African Football League utafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 20 saa 12 jioni na tayari viingilio vimewekwa hadharani. Katika ufunguzi huo tutashuka dimbani kuikabili Al Ahly kutoka Misri mtanange ambao tunaamini utakuwa mgumu. Eneo la VIP A halitauzwa tiketi zake sababu limeandaliwa kwa ajili ya Viongozi mbalimbali kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) pamoja na FIFA. Hivi hapa viingilio vyenyewe Platinum Sh. 200,000 VIP B Sh. 40,000 VIP C Sh. 30,000 Orange Sh. 10,000 Mzunguko Sh. 7000 Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwenye mtandao na Vituo ziatakapokuwa zinauzwa vitatangazwa muda wowote kutoka sasa.
Advertisement
Back to homepage
Share this story