Simba Sports Club
News

Hivi hapa viingilio vya mchezo wa Simba, Yanga

30 Oct 2023 By simbasc 245 views
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally ametangaza viingilio vya mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya watani wetu Yanga utakaopigwa Jumapili, Novemba 5 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Ahmed amesema viingilio vimetangazwa wiki moja kabla ili kuwapa nafasi mashabiki kununua tiketi mapema kuepuka usumbufu. Sisi ndio wenyeji wa mchezo na tayari tumeweka hadharani viingilio ambavyo ni rafiki ili kuwafanya mashabiki kujitokeza kwa wingi. Viingilio ni kama ifuatavyo: Mzunguko Sh. 5,000 Vip A Sh. 40,000 Vip B Sh. 30,000 Vip C Sh. 20,000 Orange Sh. 10,000 Platinum Sh. 150,000 Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kupitia kwenye mitandao na vituo ambavyo zitaanza kuuzwa vitatangazwa muda wowote kutoka sasa.
Advertisement
Back to homepage
Share this story