Ahmed amesema Viingilio hivyo vimezingatia umuhimu wa mchezo kwakuwa tayari tumetolewa ingawa kwetu tunataka kuweka heshima.
Ahmed amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani licha ya kuwa hatuendi popote lakini msimu huu kwenye hatua ya makundi hatujapata ushindi wowote kwahiyo hasira zetu zitaishia kwa Stade Malien Jumamosi.
"Ombi langu ni moja kwa Wanasimba, tunafahamu kwamba mechi hii hata tukishinda hakuna mahala tunakwenda lakini kushinda ni muhimu sababu unatengeneza kujiamini kwa wachezaji kuelekea mechi iliyopo huko mbele.
"Bado tuna vita kubwa kwenye Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ili tujiamini huko mbele lazima tushinde mechi hii, tumewafunga Mashujaa na KMC lakini watu bado hawajaridhika, sasa mechi hii ni muhimu kushinda ili kuonyesha kwamba tumeimarika," amesema Ahmed.
Hivi hapa Viingilio vya mchezo dhidi ya Stade Malien
Mzunguko - Tsh. 3,000
VIP C - Tsh. 5,000
VIP B - Tsh. 10,000
VIP A - Tsh. 20,000
Platinum - Tsh. 100,000