Ahmed ametangaza Viingilio hivyo wakati akizindua Tawi la Wekundu wa Kurasini Mji mpya ikiwa pia ni sehemu ya hamasa kuelekea mchezo huo muhimu ambao tunakiwa kupata alama tatu.
Ahmed ameweka wazi kuwa kutokana na umuhimu wa alama tatu katika mchezo huo tumeamua kuweka Viingilio rafiki ili mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu.
"Tumeamua kuweka Viingilio vidogo kwakuwa hiki ndicho kipindi ambacho tunawahitaji sana mashabiki kwakuwa tunahitaji ushindi na tunacheza na timu ngumu," amesema Ahmed.
Hivi hapa Viingilio vilivyotangazwa:
Mzunguko Shilingi 3000
Advertisement
VIP C Shilingi 5000
VIP B Shilingi 10,000
VIP A Shilingi 20,000
Platinum Shilingi 100,000
Tanzanite Shilingi 150,000 (Zimeisha).