Simba Sports Club
News

Hivi hapa Viingilio vya mchezo dhidi ya Constantine

13 Jan 2025

Meneja Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema ingawa tayari tumefuzu robo fainali lakini tunahitaji kushinda ili kuongoza kundi ndio maana tunahitaji nguvu ya mashabiki.

Ahmed amesema faida yakuwa kinara wa kundi ni kuanzia ugenini kwenye mechi za robo fainali na kumalizia nyumbani hivyo kuwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Ahmed ameongeza kuwa imebidi kutangaza viingilio wiki moja kabla ili mashabiki wanunue mapema kwakuwa tunawahitaji sana Benjamin Mkapa siku ya Jumapili.

"Ni kweli tumefuzu kuingia robo fainali lakini tunahitaji kushinda dhidi ya CS Constantine kwakuwa tunahitaji kuongoza kundi. Viingilio tayari vimetangazwa na sitegemei kuona Mwanasimba anakosekana Benjamin Mkapa siku ya Jumapili," amesema Ahmed.

Hivi hapa Viingilio vilivyotangazwa:

Mzunguko Sh. 5000

Advertisement

Machungwa Sh. 10,000

VIP C Sh. 15,000

VIP B Sh. 20,000

VIP A Sh. 30,000

Platinum Sh. 150,000

Tanzanite Sh. 250,000

Back to homepage
Share this story