Simba Sports Club
News

Hivi hapa Viingilio vya mchezo dhidi ya Bravo

20 Nov 2024

Viingilio hivyo vimetangazwa mapema na pia ni rafiki kwakuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunaujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewaomba mashabiki wetu kununua tiketi mapema ili kupunguza usumbufu katika siku ya mchezo.

Ahmed ameongeza kuwa malengo ya klabu ni kuhakikisha tiketi zinamalizika siku mbili kabla ya mchezo.

"Viingilio tayari tumevitangaza na tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao, tunachowaomba Wanasimba ni kununua tiketi mapema ili kuujaza Uwanja mapema," amesema Ahmed.

Hivi hapa Viingilio vya mchezo:

Advertisement

VIP A 50,000

VIP B 20,000

VIP C 15,000

Machungwa 10,000

Mzunguko 5,000

Back to homepage
Share this story