Viingilio hivyo vimeangalia hali halisi ya vipato vya mashabiki wetu ambapo cha chini kitakuwa Shilingi 5,000.
Lengo letu ni kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi na kuujaza Uwanja wa Mkapa kama kawaida yetu tunapocheza michuano ya kimataifa.
Kama kawaida kabla ya kuanza kwa mchezo kutakuwa na burudani mbalimbali ambazo zitaanza kutangazwa wiki hii, jambo la muhimu tunawaomba Wanasimba kujitokeza kwa wingi uwanjani.
Tumeshinda mchezo wa kwanza ugenini lakini bado hatujafuzu hivyo Wanasimba tunawaomba mjitokeze kwa wingi kuisapoti timu na tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao.
Viingilio hivyo ni kama ifuatavyo:
Mzunguko Sh 5,000
Advertisement
Machungwa Sh 7,000
VIP C Sh 10,000
VIP B Sh 20,000
VIP A Sh 30,000
Platinum Sh 150,000