Simba Sports Club
News

Hitimana amvulia kofia Ajibu

4 Nov 2021

Kaimu Kocha Mkuu Hitimana Thierry, amemwagia sifa kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu kwa kiwango bora alichoonyesha katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC.

Ajibu aliingia kipindi cha pili na kuongeza ufundi katika idara ya ushambuliaji kwa kupiga pasi na kuwafungua Namungo ambao muda mwingi walikuwa wanazuia.

Hitimana amesema Ajibu ni mchezaji mzuri ingawa hajapata nafasi kubwa ya kucheza lakini kwa kuwa bado tuna mechi nyingi na mashindano mbalimbali atazidi kuonekana uwanjani.

Advertisement

"Ajibu ni mchezaji mzuri, ana kipaji kikubwa, tulimuingiza baada ya kuona Namungo wanacheza nyuma ili akawafungue pia tuliona wanacheza sana faulo na Ajibu ni mzuri kwenye mipira ya adhabu tulijua atatusaidia na kweli ametimiza malengo yetu," amesema Hitimana.

Katika mchezo wa jana Ajibu ndiye aliyeanzisha mpira wa adhabu kwa Mohamed Hussein ambaye alipiga krosi iliyounganishwa kwa kichwa na Medie Kagere na kutufungia bao la ushindi.

Back to homepage
Share this story