Simba Sports Club
News

Historia kubwa kuhusu uwanja wa 11 Novemba

7 Feb 2026

Rekodi hiyo iliwekwa na Messi November 14, 2025 Messi alifunga bao la kwanza katika ardhi ya Afrika kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Angola.

Mchezo ulipigwa Uwanja wa November 11, hapa Luanda Angola na Messi kuweka rekodi hiyo ya kufunga bao la kwanza Afrika dakika 81, katika maisha yake yote ya soka.

Mechi hiyo iliyomalizika kwa Argentina kushinda mabao 2-0, dhidi ya Angola huku bao lingine likifungwa na Lautaro Martínez kipindi cha kwanza dakika 44.

Messi amewahi kuwa mshindi wa mchezaji bora wa dunia (Ballon D’or) mara nane (8) na tuzo nyingine nyingi.

Uwanja huu ambao Messi ameweka rekodi hiyo Mnyama Simba kesho Februari 7, 2026 atakuwa hapa kucheza mchezo wa tano Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Petro Atletico kuanzia saa 11:00 jioni ya hapa na saa 1:00 usiku kwa saa ya Afrika Mashariki.

Advertisement

Messi akiweka rekodi hiyo Mnyama Simba nae anarekodi ya kuvutia katika Uwanja huu. Rekodi ya kwanza ya Simba bao la mwisho ndani ya uwanja huu lilifungwa na Wajina wake Messi (Lionel Ateba) katika sare ya bao 1-1, dhidi ya Bravos mchezo wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

Lionel Ateba kwa sasa si sehemu ya kikosi cha Simba.

Rekodi nyingine Simba katika Uwanja huu haijapoteza mchezo wowote kwani kwa mara ya kwanza kucheza hapa ilikuwa Oktoba 9, 2022 katika mchezo wa kufudhu hatua ya makundi Ligi ya mabingwa Afrika mzunguko wa pili.

Simba ilishinda mabao 3-1, dhidi ya Primeiro de Agosto yaliyofungwa na Clatous Chama aliyopo kikosini kwa sasa na mengine mawili Moses Phiri na Israel Mwenda.

Mnyama Simba anakwenda kutafuta rekodi nyingine kesho katika mchezo wa tano Ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Petro.

Back to homepage
Share this story