Simba Sports Club
News

Hii hapa ratiba kamili ya Tembo Card Simba Matawi Bonanza 2025

3 Sep 2025

Bonanza la Simba Day litafanyika Jumamosi ya Septemba 5 katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es kuanzia saa nne asubuhi.

Matawi 22 yamethibitisha kushiriki na kila mmoja tayari ameshafahamu atacheza na nani kwenye mechi ya kwanza baada ya droo kukamilika.

Hii hapa ratiba kamili iliyopangwa baada ya kukamilika kwa droo.

1. Simba Hatari vs Home Boys (Wazo Hill)

2. Wababe wa Kimataifa vs Simba Maendeleo (Lumo)

3. Wekundu wa Kibamba vs Wekundu wa Mtogole

4. Mpira Maendeleo vs Simba Damu Fans (SDF)

5. Mpira Pesa Group vs Wekundu wa Chamazi

Advertisement

6. Vuvuzela vs Nguvu ya Simba Asilia

7. Wakwanza Sisi (Mbagala) vs Wekundu wa Terminal

8. Mpira Pesa Mikumi vs Karume Unstoppable

9. Ukonga Mazizini vs Kapu la Magoli

10. KRM vs Tunawakera

11. Asili ya Simba (Kawe) vs Mtongani

Bingwa wa Tembo Card Simba Matawi Bonanza atajinyakulia pesa taslimu Shilingi milioni mbili (2,000,000) Kombe pamoja na medali wakati mshindi wa pili akijipatia Shilingi milioni moja (1,000, 000) na medali.

Back to homepage
Share this story