Simba Sports Club
News

Hatutaingia kinyonge kwa Mkapa Jumapili

16 Sep 2022

Ahmed ameyasema hayo wakati akizunguka mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam kuanzia Tawi la Mpira Pesa lililopo Magomeni Mikumi, Soko la Magomeni, Manzese mpaka Mabibo Sokoni kwa ajili ya hamasa, kuuza tiketi na jezi.

Ahmed amesema mashabiki waje kwa wingi Jumapili wakiwa na uhakika wa kushuhudia kandanda safi kutoka kwa vijana wa Kocha Juma Mgunda.

Advertisement

"Tukiwa nyumbani hatuingii kizembe, lazima wapinzani wajue kwamba wamefika Tanzania, wapo nyumbani kwa Mnyama. Tutafanya balaa kubwa zaidi, Hatujamalizaaaa,” amesema Ahmed Ally.

Tutaingia kwenye mchezo huo tukiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa nchini Malawi Jumamosi iliyopita.

Back to homepage
Share this story