Hategekimana (47) amejiunga nasi akitokea AS Kigali ya nchini kwao Rwanda.
Hategekimana amefuzu mafunzo ya kozi mbalimbali za viungo kwa wachezaji, ana Diploma ya Uongozi wa Michezo, Mkufunzi wa viwango (GPS) kwa wachezaji, Kozi ya juu ya Viungo inayotolewa na FIFA aliyopata Oktoba 2018 Johannesburg, Afrika Kusini.
Wasifu wa Hategekimana kabla ya kutua kwetu...
- Agosti 2022 hadi sasa, Kocha wa Viungo AS Kigali, ambapo ameshinda taji la Super Cup.
- 2021-2022 Kocha wa Viungo Polisi Rwanda.
- 2021 Kocha wa Viungo wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Rwanda.
- 2019-2021 Kocha wa Viungo wa AS Kigali.
- 2018 Kocha wa Viungo wa timu ya Taifa ya Rwanda chini ya umri wa miaka 23.
- 2017-2018 Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha wa Viungo wa Rayon Sports, na ameshinda taji la Ligi pamoja na kufika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
- 2016-2017 Kocha wa Viungo ISONGA Academy FC.
- 2015 mpaka sasa ni Mkufunzi wa CAF katika Sayansi ya Viungo.
- 2007-2017 Mwalimu wa Viungo IFAK Secondary School.
- 2009-2018 Mkurugenzi wa Ufundi katika Shule ya Gasabo.
- 2014-2015 Kocha wa Viungo wa Kiyovu FC.