Hamza alipata majeraha katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 16 mwaka huu.
Baada ya upasuaji huo kukamilika na kufanikiwa Hamza ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari mpaka atakapopata nafuu na kurejea uwanjani.
Advertisement
Bado haijafahamika Hamza atakaa nje kwa muda gani baada ya kukamilika kwa upasuaji huo ambapo jopo la madaktari litaendelea kufuatilia maendeleo yake hadi atakapopona.
Kliniki ya Zerktouni ndio sehemu ambayo mlinda mlango wetu Moussa Camara alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi uliopita na sasa anaendelea vizuri.