Simba Sports Club
News

Hakuna mchezaji mwenye Covid-19

4 Dec 2021

Majibu ya vipimo vya Covid-19 yametoka na hakuna mchezaji yeyote kati ya 25 waliosafiri aliyekutwa na maambukizi hayo.

Majibu hayo yametolewa katika kikao cha maandalizi ya mchezo (Pre match meeting) kilichofanyika katika Ofisi za Chama cha Soka nchini Zambia muda mfupi uliopita.

Advertisement

Hadi muda huu hakuna dalili zozote kutoka kwa wapinzani wetu Red Arrows kutufanyia hujuma au figisu zozote za nje ya uwanja.

Back to homepage
Share this story