Timu yetu imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa jumla ya mabao 4-2 dhidi ya Red Arrows baada ya mechi zote mbili.
Kikosi kimeshuka katika Uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka, Zambia kuikabili Arrows na kupoteza kwa 2-1 lakini tumepita kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga sababu ya ushindi mnono tuliopata nyumbani mwishoni mwa mwezi Novemba.
Advertisement
Tumekuwekea picha za matukio mbalimbali wakati mchezo huo ukiendelea.