Gor Mahia ni timu ambayo tunategemea itatupa upinzani mkubwa na itakuwa kipimo sahihi kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa mashindano.
Mchezo huo utawapa nafasi mashabiki wetu kuiona timu yao ambayo itatuwakilisha kwenye michuano yote tutakayoshiriki kwenye msimu huu mzima wa 2025/2026.
Advertisement
Huu ni utaratibu ambao tumeweka kualika timu kutoka nje kwa ajili ya kushiriki kwenye kilele cha Simba Day lengo likiwa kukipima kikosi chetu kabla ya kuanzia mashindano.
Kikosi chetu kinarejea leo kutoka nchini Misri kilipokuwa kimeweka kambi ya maandalizi kwa siku 28.