Simba Sports Club
News

Gomes: Nimetazama mechi nane za Mtani, najua jinsi ya kuwakabili

1 Jul 2021 By simbasc 891 views

Kocha Mkuu Didier Gomes, amesema ameangalia kwa makini mechi nane za watani wetu Yanga ambao tutakutana Jumamosi hii hivyo anajua jinsi ya kuwakabili.

Gomes amesema katika mchezo wa mzunguko wa kwanza aliona mapungufu yetu na wao kama benchi la ufundi wamejitahidi kuyafanyia kazi.

Amesema kuna wachezaji Yanga wana uwezo mkubwa lakini hatutaingia kwa kuangalia mchezaji mmoja mmoja badala yake tumejipanga kuikabili timu nzima.

Advertisement

"Nimezitazama mechi zao nane za karibuni hivyo kuna vitu tumeviona ambavyo tunaamini vitatusaidia kupata ushindi, tunajua mechi itakuwa ngumu lakini tupo tayari kupambana," amesema Gomes.

Gomes amekiri licha ya ugumu uliopo kwenye mechi hiyo lakini lengo ni moja tu kuhakikisha tunapata ushindi ili hatimaye tuchukue ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

Back to homepage
Share this story