Kocha Mkuu Didier Gomes amesema tutaingia katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili dhidi Jwaneng Galaxy kwa tahadhari bila kuwadharau wapinzani.
Gomes amesema Galaxy siyo timu kubwa kama yetu lakini kwenye mpira wakati mwingine kuna matokeo ya kushangaza hivyo tutaingia kwa tahadhari.
Gomes amesema kutokana na ukubwa wa Simba ndiyo maana msimu uliopita tulikuwa miongoni mwa timu nane bora Afrika lakini ili kuwa na mwendelezo bora tunapaswa kuvuka hatua hii na kuingia makundi.
"Nimeitazama Galaxy kupitia video ni timu nzuri, inashambulia kwa kasi pia wanazuia kwa pamoja kwa hiyo tunapaswa kuwa makini kuwadhibiti hatutakiwi kufanya makosa mengi ya ulinzi.
"Malengo yetu ni kufika hatua ya makundi kwa hiyo inabidi tuchukue tahadhari zote bila kuangalia ukubwa wetu hatutaidharau Galaxy," amesema Gomes.