Kocha Didier Gomes amesema mshambuliaji Chris Mugalu na kiungo Ousmane Sakho bado hawajaanza mazoezi pamoja na wenzao kutokana na kuendelea kuuguza majeraha.
Gomes amesema wawili hao wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa daktari ili kuangalia kama watakuwa tayari kabla ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana wiki ijayo.
Amesema Kiungo Sadio Kanoute na Mlinzi Shomari Kapombe wamerejea mazoezini na leo wamecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Cambiaso Sports baada ya kupona majeruhi.
"Kanoute na Kapombe tayari wamerejea mazoezini bado Mugalu na Sakho, tutaendelea kufuatilia afya zao ili tujue kama tutaweza kuwatumia katika mchezo ujao dhidi ya Galaxy au la," amesema Gomes.
Wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa wataanza kuripoti mazoezini kesho kuendelea na programu ya mwalimu.