Simba Sports Club
News

FULL TIME : Zira FC 1-1 Simba SC

24 Jul 2023

Fuatilia moja kwa moja Updates za mchezo huu kuanzia dakika ya kwanza hadi mwisho ili kujua kila kinachoendelea.

Tayari kikosi kitakachoanza kimepangwa na kitakuwa ifuatavyo:

Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Henock Inonga (29), Che Malone (6), Mzamiru Yassin (19), Kibu Denis (38), Sadio Kanoute (13), Willy Onana (7), Said Ntibazonkiza (39), Moses Phiri (25).

Wachezaji wa Akiba

Ahmed Feruzi (31), Jefferson Luis, (30) Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Fabrice Ngoma (23), Aubin Kramo (24), Clatous Chama (17), John Bocco (22), Mohamed Mussa (14), Peter Banda (11). Jimmyson Mwanuke (21)

Dakika ya Kwanza - ZIra FC 0-0 Simba SC

Dakika ya "5" - Mpira umeanza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa kasi

Dakika ya “10” - Mpira wa kasi sana Timu zote zikishambuliana kwa zamu

Dakika ya “15” - Tunafanya shambulizi kali Krosi ya Shomari Kapombe inaokolewa na mabeki wa Zira

Dakika ya “19” - Zira wanapata penati baada ya mshambuliaji wao kufanyiwa madhambi ndani ya bosi

Dakika ya “19” - Zira wanakosa penati Ally Salim anaokoa mpira uliopigwa na Filip Pahtmann

Dakika ya “25” - Mpira umesimama dakika 1 (Water Break)

Dakika ya “30” - Shuti kali la Kibu Denis linaokolewa na Kipa wa Zira Tyaqo Silva

Dakika ya “33” - Kibu Dennis anatuandikia bao la kwanza kwa shuti kali akipokea pasi nzuri ya Saido Ntibazonkiza

Advertisement

Dakika ya “40” - Simba wanalishambulia goli la Zira

Mapumziko - Zira FC 0-1 Simba SC (Mfungaji Kibu Dennis pasi ya mwisho Said Ntibazonkiza)

Mabadilko - Moses Phiri anatoka anaingia Aubin Akramo

Dakika 46 - Kipindi cha pili kimeanza

Dakika “50” - Mpira unachezwa na Kasi Zira wanapata kona mlinda mlango Ally Salim anaokoa vizuri

Dakika “60” - Zira wanafanya mabadiliko ya wachezaji 8

Dakika “63” - Zira wanasawazisha kupitia Rustam Ahmadzade kwa kuunganisha krosi ya Fuad Bayramov (Simba 1-1 Zira FC)

dakika "65" - Anatoka Onana anaingia Clatous Chama

Dakika "75" - Nahodha John Bocco anaingia akichukua nafasi ya Akramo

Dakika “80” - Kibu Dennis anakosa goli la wazi kabisa

Dakika "85" - Mpira uko na kasi huku Simba wakishambulia sana

Dakika "86" - Anaingia Fabrice Ngoma na Israel Mwenda anatoka Kibu Dennis na Sadio Kanoute

Mpira umekwisha - Zira FC 1-1 Simba Sc

Back to homepage
Share this story