Simba Sports Club
News

FULL TIME : Telecom 1-2 Simba

28 Jul 2024

Dakika ya kwanza - Telecom 0-0 Simba SC

Dakika ya 10 - Mechi inaendelea kila timu ikipiga pasi haswa upande wake.

Dakika ya 15 - Shuti la Karabaka linatolewa na kipa wa Telecom na kuwa kona

Dakika ya 18 - Telecom wanapata bao la kuongoza lililofungwa kwa kichwa na Ashour Shika, aliyeunganisha mpira wa krosi.

Dakika ya 30 - Mapumziko mafupi (Water Break)

Dakika ya 35 - Mchezo unaendelea tumerudi kwa kasi

Dakika ya 42 - Karabaka anapoteza nafasi ya wazi akiwa ndani ya boksi baada ya kupiga shuti lililotoka nje. Karabaka alikutana uso kwa uso na na kipa wa Telecom Karabaka alipokea pasi kutokea kwa Hamza.

Mapumziko - Telecom 1-0 Simba

Kipindi Cha pili kimeanza - Telecom 1-0 Simba mabadiliko anatoka David Kameta anaingia Kelvin Kijili

Dakika ya 47 - Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi

Dakika ya 53 - Krosi safi ya Kijili anamkuta, Fredy ndani ya boksi akiunganisha kwa mguu wa kulia na kipa wa Telecom anapangua na kuwa

Advertisement

Dakika ya 58 - Mabadiliko anatoka Freddy anaingia Valentino Mashaka

Dakika ya 62 - Shambulizi zuri kutokea nyuma linamkuta, Nouma aliyekuwa pembeni kushoto na kupiga krosi nzuri ya chinichini na kumkuta, Mashaka aliyefunga bao la kusawazisha.

Mabadiliko Anatoka - Okejepha na Anaingia - Awesu Awesu

Dakika ya 65 - Mchezo unaendelea Telecom 1-1 Simba

Dakika ya 71 - Mabadiliko Anatoka - Chasambi Anaingia - Onana

Dakika ya 78 - Mechi inaendelea tunawapelekea mashambulizi, Telecom na tunamiliki mpira muda mwingi huku Telecom wakionekana kupoteza muda.

Dakika ya 80 - Mpira unaendelea huku tukiwashambulia Telecom wamepaki basi

Dakika 87. Anatoka - Nouma na Anaingia - Chasambi

Dakika ya 88 - Krosi nzuri ya Kijili inamkuta Chasambi aliyekuwa ndani ya boksi na kuunganisha kwa (Semi-Volley) na kufunga bao la pili.

Mpira umemaliza - Telecom 1-2 Simba

Back to homepage
Share this story