Tutakuwekea updates za kila kitakachokuwa kinaendelea katika mchezo huo kupita hapa kwenye App yetu.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
1. Ally Salim 2. Israel Patrick 3. Gadiel Michael 4.Joash Onyango 5. Henock Inonga 6. Victor Akpan 7. Moses Phiri 8. Jonas Mkude 9. Habibu Kyombo 10. Clatous Chama 11. Augustine Okrah
Kick Off - Simba SC VS Abo Hamad
05 - Simba SC 0-0 Abo Hamad
07 - Tunapata kona Israel Mwenda anaenda kupiga
10 - Tunapata Faulo nje ya 18 Okrah anaenda kupiga
15 - Simba SC 0-0 Abo Hamad
20 - Bado milango yote migumu
22 - Gadiel anakosa goli baada y Kipa wa Abo Hamad kuokoa
24 - Abo Hamad wanapata Offside ya Kwanza
26 - Mpira unachezwa katikati ya Uwanja mbinu zikitawala
27 - Okrah anafanyiwa madhambi mpira umesimama akipatiwa matibabu
28 - Mpira unaendelea Okrah amerudi Uwanjani
30 - Huyu Okrah ni hatari Simba Day Ifike tu na nyinyi mje muone wenyewe
35 - Tunapata Kona mpigaji ni Okrah ngoja nikae vizuri
37 - Mpira unachezwa sana kati Hapo Akpan na Mkude wamelimilika vyema Dimba
42 - Bado dakika 3 Mapumziko magoli magumu
44 - Moses Phiri anatuinua vitini baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Clatous Chama
Mpira ni mapumziko Simba 1-0 Abo Hamad
Kipindi cha Pili - Wanatoka - Moses Phiri, Victor Akpan, Henok Inonga , Clatous Chama na Habib Kyombo
Wanaingia - Erasto Nyoni, Jimmyson, Ouattara,Banda, na Chris Mugalu
46 - Kipindi cha pili kinaanza
55 - Tunaongoza bao 1-0
57 - Tunapata bao la pili likifungwa na Kiungo Jonas Mkude pasi kutoka kwa Okrah
58 - Tunaongoza 2-0
59 - Wanatoka - Gadiel, Mkude, Mwenda, na Okrah
- Wanaingia - Taddeo, Kapama, Sakho, na Kagere
69 - Kifaru cha Kinywaranda Medie Kagere anatuinua baaada ya kupokea pasi nzuri ya Wonderkid Peter Banda
71 - Goli la nne Pape Sakho anatuinua goli la Caf
75 - Simba 4 - 0 Abo Hamad
80 - Banda na Sakho wanagongeana zinapigwa pasi nyingi katikati ya Uwanja
86 - Sakho anafunga goli la pili akipokea asist ya Banda
87 - Mchezo unaendelea tukiliandama lango lao
90 - Erasto Nyoni anatufungia goli la 6
Mpira umemalizika - Simba SC 6-0 Abo Hamad