Simba Sports Club
News

FULL TIME: Simba SC 3-0 Namungo FC

1 Oct 2025

Kikosi kinachoanza - YAKOUB, KAPOMBE, MLIGO, CHAMOU, DE REUCK, KAGOMA, MPANZU, KANTE, MUKWALA, MORICE MUTALE

Kikosi kikipasha misuli moto.

Tayari timu imesharudi vyumbani baada ya kupasha misuli moto muda wowote kuanzia sasa mchezo utaanza.

Mchezo umeanza - Simba SC 0-0 Namungo FC

Dakika ya 3 - Tunawashambulia kwa kasi.

Dakika ya 6 - Chamou anafunga goli mwamuzi anasema ameotea

Dakika ya 8 - Abdallah Mfuko anaoneshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Elie Mpanzu

Dakika ya 9 - Zinapigwa moja mbili tatu morice na mutale lakini Namungo wapo imara kuzuiya

Dakika ya 11 - Makambo anashindwa kuendelea na mchezo anaingia fabrice Ngoy

Dakika 20 - Tunawashambulia sana golini kwao mpira mzuri kabisa

Dakika 30 - Budo anapiga shuti kali linaokolewa na golikipa wa Namungo

Dakika ya 35 - Mukwala anaunganisha mpira wa Budo unagonga mwamba nakurudi uwnajani

Dakika ya 44 - Budo anapiga kona inaunganishwa vizuri kwa kichwa na Inspekta Karaboue Chamou

Dakika 2 za Nyongeza

Mpira umesimama nahodha Shomari Kapombe anatibiwa baada ya kuchezewa madhambi

Advertisement

Mpira ni Mapumziko - Simba SC 1-0 Namungo FC

Simba wamefanya mabadiliko anatoka Elie Mpanzu na Kuingia Neo Maema

Kipindi cha pili kimeanza

Dakika ya 55 - Simba Sc 1 -0 Namungo FC

Dakika ya 61 - De Reuck anafunga goli la pili kwa krosi ya Neo Maema

Dakika ya 69 - Anatoka Mukwala na. Morice anaingia Ahoua na Mwalimu

Dakika ya 80 - Kante na Budo wanaenda nje anaingia Semfuko na Kibu Denis

Mpira unachezwa kati kati ya uwanja Simba wakimiliki kwa asilimia kubwa

Dakika ya 82 - Mligo anapewa kadi ya njano

Dakika ya 84 - Selemani Mwalimu anawazidi ujanja Namungo na kufunga goli la 3 Kwa Simba

Dakika ya 86 - Namungo wanapata kona inaokolewa vizuri

Dakika ya 88 - Tunagonga pasi hapa na pale burudani safi kwa Wanasimba

Dakika 3 za Nyongeza

Rushine De Reuck anaoneshwa kadi ya njano

Dakika 90 zimeisha - Simba SC 3-0 Namungo FC

Back to homepage
Share this story