Simba Sports Club
News

FULL TIME : Simba SC 1-1 FC Fassel

27 Aug 2025

Kaa Karibu na Simba app kupata live updates ya kinachoendelea

Tayari kikosi kimefika uwanjani

Wachezaji wakipasha misuli moto

Mpira umeanza - Simba SC 0-0 FC Fassel

Dakika ya 8 - Mechi inaendelea

Dakika ya 10 - Baada ya beki wa Fassel kushika mpira pembeni ya boksi inapatikana faulo inapigwa na Mutale na mpira huo unakwenda kugonga mwamba wa juu baada ya kipa wa timu pinzani kuupangua na kuwa kona.

Dakika ya 11 - Mutale anamuanzia Awesu kona fupi. Na Mutale anapiga kevi nzuri na kupanguliwa na kipa.

Dakika ya 16 - Krosi nzuri ya Mutale inamkuta Mukwala ndani ya boksi na kuunganisha mpira huo wa kichwa unatoa karibu na goli la wapinzani.

Dakika ya 17 - Hadi sasa mechi tumeiliki kwa kiasi kikubwa tunashambulia, kumiliki mpira huku Mutale akionekana kuwasumbua wapinzani.

Dakika 22 - Mechi imesimama mapumziko mafupi (Water breack)

Dakika ya 23 - Mechi inaendelea

Dakika ya 25 - Simba SC 0-0 FC Fassel

Dakika ya 27 - Pasi nzuri iliyotoka kwa Mutale inakwenda kwa Mukwala aliyekuwa nje ya boksi anawadaha mabeki wa timu pinzani na kuingia na mpira ndani ya boksi na kupiga pasi nzuri ya mwisho kwa Sowah aliyeweka mpira huo wavuni.

Dakika ya 30 - Mechi inaendelea Simba 1-0 Fassell

⚽️ Sowah

Advertisement

Dakika ya 34 - Fassell wanapata penati baada ya Hussein Mbegu kumkatana mchezaji wa timu pinzani ndani ya boksi.

Dakika 36 - Fassell wanapata bao la kusawazisha kutokana na mkwaju wa penati.

Dakika 40 - Simba SC 1-1 FC Fassell

Mapumziko

Kipindi cha pili kimeanza

Dakika ya 50 - Mpira unaendelea huku team zote zikicheza sana kati ya uwanja

Dakika ya 60 - FC Fasell wanatushambulia

Dakika ya 68 - Mabadiliko Awesu na Bashiru

Wameingia Naby Camara na Abraham

Dakika ya 75 - Krosi nzuri ya Mutale inamkuta Sowah aliyekuwa ndani ya boksi na kuunganisha mpira huo kwa mguu wa kulia na kutoka karibu na goli la wapinzani

Dakika ya 80 - Wanatoka Mukwala na Sowah

Wanaingia Mashaka na Kibu

Dakika 87 - Mechi inaendelea timu zote zinamiliki mpira muda mwingi katikati mwa kiwanja.

Dakika 90 zimemalizika

Back to homepage
Share this story